Kwanini maandamano ya vijana yamepunguka kasi Kenya? - BBC News Swahili (2024)

Kwanini maandamano ya vijana yamepunguka kasi Kenya? - BBC News Swahili (1)

Maelezo kuhusu taarifa
  • Author, Abdalla Seif Dzungu
  • Nafasi, BBC Swahili
  • Twitter, @SeifDzungu
  • Akiripoti kutoka Nairobi Kenya

Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga alikuwa akikabiliana na shutuma kutoka kwa vijana kuhusu pendekezo lake la kushiriki mazungumzo ya kushughulikia masuala yaliyoibuliwa na Gen Z wakati wa maandamano dhidi ya serikali.

Wakati wa kutiwa saini kwa sheria ya katiba ya IEBC 2024, katika jumba la kimataifa la KICC mjini Nairobi, Rais William Ruto alitangaza kongamano la kitaifa la siku sita kushughulikia masuala yaliyoibuliwa na waandamanaji hao.

Hata hivyo nia ya kiongozi huyo wa Azimio kushiriki katika mazungumzo hayo ilizua hisia za wananchi, huku vijana wakimshutumu kwa ‘kuegemea upande wa serikali.’

Katika barua iliyopewa jina la ‘Agwambo Kaa Home’ iliyoandikiwa Odinga na Gen Z, vijana hao walieleza kusikitishwa kwao na uamuzi wa Odinga.

Hata hivyo kadiri siku zilivyosonga, kiongozi huyo alipata kuungwa mkono na viongozi wa kidini ambao mara kwa mara waliwataka Gen Z kuruhusu mazungumzo ya kitaifa ambayo yangeshughulikia masuala yao..

Pia unaweza kusoma
  • Mapendekezo ya ushuru ya Kenya ambayo yamesababisha maandamano

  • Sura mpya za maandamano - Wanamapinduzi wa Kenya wa Gen Z wanaopinga kodi

  • William Ruto: Rais 'mtoza ushuru' anayezua hasira za Wakenya

Mazungumzo ya Rais William Ruto na Raila Odinga

Lakini huku hasira dhidi ya Raila Odinga ikiendelea, mazungumzo ya kisiri kati ya kiongozi huyo na Rais Ruto yalipelekea viongozi wanne wa upinzani kutoka chama cha ODM{ chama kinachoongozwa na Raila} kujiunga na Serikali.

Wanne hao sasa wamechaguliwa kuwa mawaziri katika Baraza jipya la Mawaziri baada ya Baraza la awali kuvunjwa na rais kufuatia shinikizo kutoka kwa Gen z .

Kulingana na wachambuzi wa kisiasa, uteuzi wao ulikusudiwa haswa kufurahisha maeneo yao ambayo wanadai kuwachwa nyuma katika ugavi wa raslimali za serikali.

Akizungumza jijini Nairobi Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alinukuliwa akisema kuwa Rais Ruto alimwomba msaada ili kuzuia makali ya vuguvugu la Gen Z ambalo lilikuwa likitishia kuiangusha serikali yake.

Raila alifichua jinsi watu wenye nyadhfa kuu seikali walivyompigia simu wakimrai kuisaidia serikali kuendesha nchi kwa ufanisi.

"Jamaa walikuwa wamelemewa na kazi wakawafuta kazi Mawaziri wote , halafu walikuja wakipiga magoti wakiomba tuchangie baadhi ya watu," Raila alifichua.

Hatua ya Raila kuchangia baadhi ya wanachama wa ODM kwa Serikali imezua tafrani katika Muungano wa Azimio huku baadhi ya wanachama wakiomba chama cha ODM kujiondoa katika muungano huo.

Licha ya kusisitiza kuwa chama hicho kiko kikamilifu katika muungano wa upinzani na kwamba wanaojiunga na Serikali wanafanya hivyo kibinafsi, wanachama wa muungano huo walisema kuwa hawana imani tena na chama hicho na kwamba kiongozi wao mpya sasa ni Kalonzo Musyoka.

Mara tu baada ya uteuzi huo, watu waliohojiwa katika ngome za ODM za Pwani, Magharibi na Nyanza walisherehekea wakisema Serikali imefanya kile kilichohitajika kufanywa miaka miwili iliyopita kwa kuruhusu mikoa yote kuwa na uwakilishi sawa.

Na kwa upande mwingine, wale waliohojiwa waliwataka wenzao kusimamisha maandamano na kumpatia rais muda zaidi kufanyia kazi masuala yaliyotolewa na Gen Z.

Hili lilithibitishwa na maandamano ya ‘Nane Nane’ ambayo kwa kiasi kikubwa yalishindwa kufanikiwa katika maeneo mengi ya nchi, huku vijana kutoka Pwani, Nyanza na Magharibi wakiyapuuza.

Hata hivyo mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Macharia Gaitho alipinga kwamba wanasiasa wamechangia pakubwa kutuliza joto la kisiasa lililopo nchini.

''Serikali inapiga hatua mbili mbele kwa kuondoa muswada wa sheria ya fedha na kulifuta baraza la mawaziri lakini sasa imepiga hatua tatu nyuma''.

‘’Ninamwona Ruto kwenye kampeni akiahidi madaraja na barabara kuu kila mahali anapoenda Taita Taveta, Mombasa, anaendesha kampeni kwa ahadi zile zile za zamani ambazo zilimvunjia heshima'', alisema Mwandishi huyo maarufu.

‘’Tabaka la Kisiasa haliwezi kudhibiti mabadiliko ya Kenya, ni 'bomu' ambalo huenda likalipuka wakati wowote ‘’, alisema bwana Gaitho katika kipindi kimoja cha redio cha KTN.

Utekaji nyara wa viongozi wa Gen z

Wakenya wamekuwa wakionyesha wasiwasi wao kuhusu visa vya utekaji nyara vinavyoongezeka nchini vinavyohusishwa na maandamano yanayoendelea kupinga serikali ya rais William Ruto.

Haya yanajiri baada ya Wakenya wanaoaminika kuongoza maandamano hayo kutekwa nyara kiholela na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi kabla ya kupelekwa maeneo yasiojulikana.

Baadhi ya vijana hao wamedaiwa kuuawa na wengine wakiachiliwa baada ya maandamano.

Baadhi ya vijana ambao wamenusurika utekaji nyara wamekuwa wakisimulia visa vya kuhuzunisha ndani ya magari ya watekaji wao huku wakiwa wamezibwa macho na kufungiwa kati ya wanaume ambao huwatisha kwamba wangewadhuru.

Licha ya baadhi ya vijana hao kusema kwamba hawatatishika na vitisho vya utekaji nyara huku wakibeba mabango yalioandikwa "Utekaji nyara hautatuzuia", baadhi yao wamehofia maisha yao na kuamua kusalia manyumbani wakati wa maandamano.

Kwanini maandamano ya vijana yamepunguka kasi Kenya? - BBC News Swahili (3)

Wahalifu waliokodishwa kuharibu maandamano

Katika eneo la katikati ya mji wa Nairobi , watu waliokodishwa wanaoendesha boda boda na waliobeba mabango yanayounga mkono serikali wamekuwa wakiwahangaisha waandamanaji .

Watu hao wanaodaiwa kutoka katika mitaa ya mabanda ya Mukuru, Kibra, Kayole na Kangemi, miongoni mwa maeneo mengine mjini Nairobi wanadaiwa kukodishwa na wanasiasa kukabiliana na maandamano ya amani .

Kana kwamba ni kwa maelekezo, maafisa wa polisi, ambao mara kwa mara wamekuwa na nia ya kuzuia maandamano katikati ya jiji, wameonekana kuwapuuza wanaume hao mara wanapowakabili vijana wa Gen Z.

Kutumika kwa risasi za moto

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekuwa likilaani unyanyasaji unaotumiwa na maafisa wa polisi dhidi ya Wakenya wanaopinga serikali.

Katika taarifa yake, Amnesty ilionyesha kuwa wandamanaji wengi walipigwa risasi za moto na kuaga dunia

Licha ya uwepo wa vitoa machozi vinavyoweza kukabili waandamanaji polisi mara kwa mara wamekuwa wakitumia risasi za moto kukabili waandamanaji.

"Tunaitaka serikali na wahusika wote kupunguza hali hiyo na kuacha kutumia nguvu kupitia kiasi na badala yake kulinda maisha ya waandamanaji," lilisema shirika hilo.

Kwanini maandamano ya vijana yamepunguka kasi Kenya? - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Peter Njoroge/BBC

Kunyamazishwa kwa vyombo vya habari

Mamlaka ya Mawasiliano nchi Kenya (CA) hivi majuzi ilivionya vyombo vya habari nchini dhidi ya kutangaza maudhui yanayohusu maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali hatua iliosema ni ukiukaji wa katiba.

Onyo hilo lilijiri kufuatia maandamano ya nchi nzima yaliosababisha ghasia, watu kupoteza maisha yao mbali na uharibifu wa mali, huku Mamlaka hiyo ikisisitiza kuwa vyombo vya habari vina jukumu muhimu la kudumisha utulivu nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa CA David Mugonyi, katika barua kwa vyumba vya habari , alisisitiza kwamba ingawa Katiba ya Kenya inahakikisha uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, haki zilizotajwa hazihusu "propaganda ya kueneza vita, uchochezi wa ghasia, chuki, au utetezi wa chuki.”

Hatua hiyo imevifanya baadhi ya vyombo vikuu vya habari ambavyo vimekuwa katika mstari wa mbele kuripoti maandamano hayo moja kwa moja nchini kusitisha hatua yao kwa hofu ya kufungiwa na serikali.

Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kueneza demokrasia nchini Kenya.

Pia unaweza kusoma
  • Jinsi zana hizi tatu zilivyotumiwa na Gen Z kuishinikiza serikali ya Kenya

  • Mapendekezo ya ushuru ya Kenya ambayo yamesababisha maandamano

  • Maelfu ya waandamanaji wasisitiza kuondolewa kwa Muswada wa fedha wa 2024 jijini Nairobi

Imeharirriwa na Yusuf Jumah

Kwanini maandamano ya vijana yamepunguka kasi Kenya? - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Pres. Carey Rath

Last Updated:

Views: 5923

Rating: 4 / 5 (41 voted)

Reviews: 88% of readers found this page helpful

Author information

Name: Pres. Carey Rath

Birthday: 1997-03-06

Address: 14955 Ledner Trail, East Rodrickfort, NE 85127-8369

Phone: +18682428114917

Job: National Technology Representative

Hobby: Sand art, Drama, Web surfing, Cycling, Brazilian jiu-jitsu, Leather crafting, Creative writing

Introduction: My name is Pres. Carey Rath, I am a faithful, funny, vast, joyous, lively, brave, glamorous person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.